Kichinjwa kimoja kinatosha hata kama mtakuwa mnaishi watu mia

Swali: Kuna mtu amekwishaoa na ana watoto na anaishi na wazazi wake na ndugu zake. Je, kichinjwa kimoja kinawatosheleza?

Jibu: Ndio, hata kama watakuwa watu mia moja kinawatosha kichinjwa kimoja. Wakiwa wamekusanyika; baba na familia yake ambapo ni watu ishirini wakiwemo wakeze kinawatosha kichinjwa kimoja. Kama watachinja vichinjwa viwili, vitatu au zaidi ya hapo hakuna neno. Lakini hata hivyo kinawatosha kichinjwa kimoja katika kuafiki Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na wake tisa na hata hivyo alikuwa akichinja kichinjwa kimoja kwa ajili yake yeye na watu wa nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3762/%D9%87%D9%84-%D8%AA%D8%AC%D8%B2%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%A7%D8%AD%D8%AF%D8%A9-%D8%B9%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%A8-%D9%88%D8%A7%D9%88%D9%84%D8%A7%D8%AF%D9%87-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%8A%D9%86-%D9%8A%D8%B9%D9%8A%D8%B4%D9%88%D9%86-%D9%85%D8%B9%D9%87-%D9%81%D9%8A-%D9%86%D9%81%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%8A%D8%AA
  • Imechapishwa: 14/08/2018