Swali: Je, inafaa kwa mtu mwenye janaba kwa mfano kuchinja kuku? Je, wudhuu´ wake unachenguka ikiwa mikono miwili imepakwa hina kwa wanamme au wanawake?

Jibu:

1 – Inafaa kwa mwenye janaba kuchinja kuku na wanyama wengineo wanaoliwa. Hakuna neno kufanya hivo – Allaah (Ta´ala) akitaka.

2 – Wudhuu´ ambaye ametawadha na mikono yake imepakwa hina unasihi. Ni mamoja akiwa mwanamme au mwanamke.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (22/375) nr. (6129)
  • Imechapishwa: 05/06/2022