Kichinjwa baada ya timu ya mpira kushinda

Swali: Wale wanaoshabikia mpira. Baadhi yao wakasema wanasema timu fulani ikishinda, basi basi kichinjwa chenu kiko juu yangu. Ni ipi hukumu ya kichinjwa hiki?

Jibu: Hili halifai, ni mamoja iwe kwa pesa au kichinjwa. Haijuzu. Hili ni miongoni mwa mkataba usiojulikana na ni kamari. Haijuzu. Wala haijuzu kwao kula kichinjwa walichochinjiwa, kwa sababu hiyo ni kamari. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ

“Enyi walioamini! Hakika si vyenginevyo pombe na kamari na kuabudu masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli ni uchafu kutokana na kazi ya shaytwaan.”[1]

Kamari ni kushindana juu ya mali, isipokuwa katika mashindano ya kurusha mishale, ya farasi au ya ngamia.

[1] 05:90-91

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31393/ما-حكم-المغالبة-على-مال-في-بعض-الالعاب
  • Imechapishwa: 24/10/2025