Khutbah ya ´iyd ni moja na haina Takbiyr

Swali: Katika ´iyd mbili muhubiri anakhubutu Khutbah mbili na katika Khutbah ya kwanza analeta Takbiyr tisa na katika Khutbah ya pili analeta Takbiyr saba. Je, hii ni Sunnah?

Jibu: Kama ilivyokuja katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy, Khutbah ni moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoa Khutbah kisha baadaye akaenda kuwakhutubia wanawake. Khutbah hii haina mwanzo wake Takbiyr; bali inatakiwa kuzungumzia yale yanayounufaisha Uislamu na waislamu.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 377
  • Imechapishwa: 05/06/2025