Allâh (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ

“Usiku wa Qadr ni bora kuliko miezi elfu.”[1]

Bi maana miezi elfu isiyokuwa na usiku wa Qadr. Usiku huo kuwa bora ni kutokana na zile thawabu kubwa za matendo anazolipwa mtu ndani yake na pia zile kheri na baraka ambazo Allaah (Ta´ala) ameuteremshia Ummah huu. Kwa ajili hiyo ndio maana akasamehewa yule mwenye kuutumia usiku huo kwa imani na kwa matarajio.

[1] 97:03

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 274-275
  • Imechapishwa: 15/05/2020