Swali: Niswali pamoja na Khatwiyb akipanda mimbari kabla ya jua kupondoka au nende katika msikiti mwingine?

Jibu: Swali pamoja naye. Maoni ya sawa ni kwamba kunasihi kufanya hivo. Zipo Hadiyth juu ya hilo. Aidha ndio madhehebu ya Hanaabilah na kikosi cha wanazuoni wengine. Lakini Khatwiyb anatakiwa aambiwe kutokwenda mapema.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 11/09/2021