Swali: Ni adhabu gani ambayo Allaah amemtishia yule atakayeshuhudia maovu na asiyabadilishe kwa ulimi wake hali ya kuwa anaweza kufanya hivyo?

Jibu: Kama Allaah alivyosema katika Suurah ”al-Maaidah”:

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ

“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa israaiyl kupitia ulimi ya Daawuud na ‘Iysaa mwana wa Maryam – hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakivuka mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.” (05:78-79)

Amewatishia laana na kufukuzwa mbali kutoka katika rehema ya Allaah. Tunamuomba Allaah atuepushe. Vilevile imekuja katika Hadiyth Swahiyh ambapo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika watu wanapoona maovu na wasiyabadilishe, basi Allaah anakaribia kuwaenezea adhabu.”

Tunamuomba Allaah atulinde.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31005/ما-حكم-من-راى-منكرا-ولم-يغيره
  • Imechapishwa: 21/09/2025