Swali: Vipi kuoanisha zile Hadiyth zinazofahamisha kuwa Khadiyjah ndiye bora kuliko ´Aaishah?

Jibu: Kuoanisha ni kwamba ´Aaishah ndiye mwanamke bora, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ubora wa ´Aaishah kwa kulinganisha na wanawake wengine ni kama ubora wa uji kulinganisha na chakula chengeni.”[1]

Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa Khadiyjah ni mbora katika wakati wake na ´Aaishah ni mbora katika wakati wake. Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa ndiye mama wa watoto wake, mwanamke wa kwanza aliyemwamini na kumsapoti. Hata hivyo ziko Hadiyth za wazi zinazofahamisha kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ndiye mwanamke bora kutokana na ile elimu na uelewa wa dini ambao Allaah alimpa. Isitoshe Allaah ameieneza elimu na Sunnah kupitia kwake. Kila mmoja katika wao anazo fadhilah zake. Wanawake bora ni watano:

1 – ´Aaishah.

2 – Khadiyjah.

3 – Faatwimah msichana wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

4 – Maryam bint ´Imraan.

5 – Aasiyaa bint Muzaahim, mkewe Fir´awn.

Lakini katika hawa tano wanawake wabora pasi na kipingamizi. Ndio wanawake wa ummah huu – Allaah awe radhi na awarehemu wote.

[1] al-Bukhaariy (3411) na Muslim (2431).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (03)
  • Imechapishwa: 03/11/2024