Swali: Mtu alipata shahada ya kielimu, lakini alighushi mitihani yake ya shahada hiyo. Pia aliwasilisha cheti cha ugonjwa cha kughushi ili apate kuingia kwenye mtihani katika moja ya miaka ya shahada hiyo. Hivi sasa anafanya kazi katika moja ya kazi kwa kutumia shahada hiyo. Je, mshahara wake ni halali au haramu? Ikizingatiwa kuwa alipewa kazi hiyo baada ya mtihani wa mdomo na akafaulu, lakini miongoni mwa masharti ya kazi ni kuwasilisha shahada hiyo ya kielimu.
Jibu: Hili ni jambo baya na kosa. Ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na asiwakilishe shahada ya udanganyifu au ya kughushi. Hili ni kosa. Ni juu yake kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Maadamu amekubaliwa katika kazi na anatekeleza majukumu yake na kuizingatia, basi hakuna tatizo juu yake katika hilo – Allaah akitaka. Asijifedheheshe, aendelee na atekeleze wajibu. Ikiwa atatekeleza wajibu wa kazi ni vyema. Lakini ni lazima kwake kutubia kwa Allaah, kujuta na kuazimia kutorudia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30965/ما-حكم-الغش-في-الشهادة-العلمية-والعمل-بها
- Imechapishwa: 22/09/2025
Swali: Mtu alipata shahada ya kielimu, lakini alighushi mitihani yake ya shahada hiyo. Pia aliwasilisha cheti cha ugonjwa cha kughushi ili apate kuingia kwenye mtihani katika moja ya miaka ya shahada hiyo. Hivi sasa anafanya kazi katika moja ya kazi kwa kutumia shahada hiyo. Je, mshahara wake ni halali au haramu? Ikizingatiwa kuwa alipewa kazi hiyo baada ya mtihani wa mdomo na akafaulu, lakini miongoni mwa masharti ya kazi ni kuwasilisha shahada hiyo ya kielimu.
Jibu: Hili ni jambo baya na kosa. Ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na asiwakilishe shahada ya udanganyifu au ya kughushi. Hili ni kosa. Ni juu yake kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Maadamu amekubaliwa katika kazi na anatekeleza majukumu yake na kuizingatia, basi hakuna tatizo juu yake katika hilo – Allaah akitaka. Asijifedheheshe, aendelee na atekeleze wajibu. Ikiwa atatekeleza wajibu wa kazi ni vyema. Lakini ni lazima kwake kutubia kwa Allaah, kujuta na kuazimia kutorudia.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30965/ما-حكم-الغش-في-الشهادة-العلمية-والعمل-بها
Imechapishwa: 22/09/2025
https://firqatunnajia.com/kazi-anayofanya-mtu-kwa-cheti-alichoghushi/