Katika hali hii ni wajibu kumkopesha ndugu yako

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa kukopesha kitu ni wajibu wakati wa haja?

Jibu: Ndiyo, wakati wa haja inakuwa wajibu, kama alivosema Allaah (´Azza wa Jall):

وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ

”… na wanazuia misaada ya kawaida kwa watu.”[1]

Mujibu wa tafsiri sahihi zaidi miongoni mwa wanazuoni wa tafsiri maana yake ni kukopesha kitu bila malipo. Wengine wamesema kuwa maana yake ni zakaah. Kwa hivyo ikiwa ndugu yako anahitaji, basi ni wajibu kwako kumkopesha Muislamu ni ndugu wa muislamu mwenzake. Kama ambavyo ni wajibu kwako kumsaidia kwa mali yako ikiwa yuko kwenye dharurah, vivyo hivyo ni lazima umpe kile kinachoweza kumuweka hai kutokana na njaa au kiu.

[1] 107:07

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25425/هل-تجب-العارية-عند-الحاجة
  • Imechapishwa: 24/03/2025