Kwa mfano mtawala ataamrisha wanajeshi wasiswali, hapa hakuna usikivu wala utiifu. Kwa sababu swalah ni faradhi ambayo Allaah ameiwajabisha kwa waja na inakuwajibikia vilevile wewe. Wewe [mtawala] ndiye namba moja unatakiwa kuswali na ambaye umefaradhishiwa swalah. Katika hali hii hasikizwi na wala hatiiwi.[1]
Lau mtawala atawaamrisha kitu cha haramu, kwa mfano kunyoa ndevu, tunasema hakuna usikivu wala utiifu. Hatumtii. Badala yake tunamtii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Ziacheni ndevu na mpunguze masharubu.”[1]
Kadhalika kila ambacho mtawala ataamrisha ikiwa ni kumuasi Allaah, hasikizwi na wala hatiiwi. Ni lazima kumuasi waziwazi na apuuzwe. Kwa sababu yule anayemuasi Allaah na akawaamrisha viumbe wamuasi Allaah, hana haki ya kusikizwa na kutiiwa.
Hata hivyo ni wajibu kumtii katika mambo mengine. Tukisema hivi ya kwamba akiamrisha maasi kumtii moja kwa moja kunaanguka. Hapana sivyo! Kutomtii inakuwa katika jambo hili kwa dhati yake ambalo ni kumuasi Allaah. Ama kuhusu mambo mengine yasiyohusiana na hilo, ni wajibu kumtii.
[1]al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/278)
- Imechapishwa: 27/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)