Katika hali hii itafaa kutumia vidonge vya kuzuia mimba kwa muda

Swali: Kumeza baadhi ya vidonge vya kuzuia mimba kunapimwa na kitendo cha kuchopoa kabla ya kumwaga manii?

Jibu: Hapana, kuna maelezo zaidi. Ni katika sababu. Kunahitaji maelezo. Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, hakuna tatizo: kama ni kwa sababu ya ugonjwa wake, ugonjwa wa tumbo la uzazi, khatari juu yake au kutokana na watoto kufuatana mno kiasi kwamba hawezi kuwalea vizuri, basi anaweza kutumia baadhi ya vidonge kwa muda fulani. Ikiwa havina madhara na madaktari wamethibitisha kuwa havina madhara na mume wake ameridhia. Kama ilivyo kuwa sababu hazizuii, vivyo hivyo vidonge havizuii, kwani akitaka Allaah jambo litokee, basi litatokea.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31652/ما-حكم-تعاطي-حبوب-منع-الحمل
  • Imechapishwa: 12/11/2025