Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na haya zaidi kuliko hata bikira aliye chumbani mwake. Pamoja na kwamba alikuwa haonelei haya haki. Kwa hiyo haya ni sifa yenye kusifika. Lakini hata hivyo usionelei haya juu ya haki. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ

“Allaah hastahi kunako haki.” (33:53)

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا

“Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake.” (02:26)

Katika haki hakuna haya. Kuwa na haya, mbali na haki, ni miongoni mwa sifa zenye kusifika. Kinyume chake ni mtu asiyekuwa na haya. Mtu kama huyu hajali kile anachofanya na wala anachosema. Ndio maana ikapokelewa katika Hadiyth:

“Hakika miongoni mwa mambo waliyokutana nayo watu kutoka katika maneno ya kiutume ni pamoja na: ikiwa huoni haya, basi fanya utakalo.”[1]

[1]al-Bukhaariy (6120).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/170)
  • Imechapishwa: 02/06/2024