Kafiri ni kafiri na mshirikina ni mshirikina

Swali: Je, kila anayetumbukia ndani ya shirki kubwa anakuwa mshirikina na zinatumika kwake hukumu za washirikina?

Jibu: Ndio, anayemkufuru Allaah anakuwa kafiri, anayemshirikisha Allaah anakuwa mshirikina. Ni kama ambavyo yule anayemuamini Allaah na Mtume wake anakuwa mpwekeshaji na muumini. Ama yule ambaye ulinganizi haujamfikia, huyu haisemwi kuwa ni muumini wala kafiri wala hataamiliwi kama muislamu. Bali jambo lake liko kwa Allaah siku ya Qiyaamah. Hao ni miongoni mwa wajinga ambao hawakufikiwa na ulinganizi. Hawa watapewa mtihani sku ya Qiyaamah. Allaah atawapelekea miale kutoka Motoni na itasemwa: ”Ingieni.” Atakayeitikia utakuwa juu yake baridi na salama, na asiyeitikia ataingia Motoni. Tunaomba kwa Allaah salama. Makusudio ni kwamba yule aliyefikiwa na ulinganizi kisha hakusadiki na hakusilimu, basi huyo ni kafiri na adui wa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3061/هل-كل-من-يقع-بالشرك-الاكبر-يكون-مشركا
  • Imechapishwa: 04/09/2025