Swali: Mnaswara akiniomba Qur-aan nimpe au nisimpe?
Jibu: Usimpe. Lakini msomee, msikilizishe, mlinganie kwa Allaah na mwombee uongofu. Amesema (Ta´ala):
وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ
“Endapo mmoja katika washirikina atakuomba umlinde, basi mlinde mpaka aweze kusikia maneno ya Allaah kisha mfikishe mahali pake pa amani.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msisafiri na msahafu katika ardhi ya adui isije kufika mikononi mwao.”
Hilo limefahamisha kwamba kafiri hapewi Qur-aan kwa kuchelea asije kuitweza au akacheza nayo. Lakini hata hivyo afunzwe, asomewe Qur-aan, aelekezwe na aombewe du´aa. Akisilimu ndio atapewa Qur-aan.
Lakini hapana neno akapewa baadhi ya vitabu vya tafsiri ya Qur-aan, baadhi ya vitabu vya Hadiyth akiona kuwa au baadhi ya tarjama za maana ya Qur-aan ikiwa kuna matarajio kuwa atanufaika kwayo.
[1] 09:06
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/444)
- Imechapishwa: 26/02/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kusafiri na Qur-aan katika nchi za makafiri
Swali: Je, inajuzu kusafiri na Qur-aan kuipeleka katika nchi ya makafiri kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakataza kusafiri na Qur-aan katika ardhi (nchi) ya maadui? Jibu: Haijuzu kusafiri kwenda na msahafu katika Bilaad-ul-Harb. Ama nchi iliyo na ahadi (mkataba) na Waislamu, hakuna neno kusafiri kwenda na…
In "Kuamini Vitabu"
48. Imamu anabeba msahafu ndani ya swalah
Swali: Ni ipi hukumu ya imamu anayebeba msahafu wakati wa swalah? Jibu: Ikiwa swalah ni ya faradhi, bora ni kutofanya hivo kutokana na kule kujishughulisha katika jambo hilo. Ikiwa swalah ni ya sunnah, kitendo hicho kinafaa. Kwa sababu swalah ya faradhi inatosha baada ya “al-Faatihah” kusoma kitu chepesi. Allaah (Ta´ala)…
In "Min Fataawaas-Swiyaam - ´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh"
Ibn Baaz kubeba msahafu katika swalah za faradhi
Swali: Je, inafaa kwa imamu katika zile swalah tano akasoma ndani ya msahafu na khaswa swalah ya Fajr? Kwa sababu kurefusha kisomo ni jambo linalotakikana na anachelea asikosee au asisahau? Jibu: Inafaa kufanya hivo haja ikipelekea kufanya hivo kama ambavo inafaa kusoma ndani ya msahafu katika Tarawiyh kwa ambaye hajahifadhi…
In "Mambo yanayochukiza katika swalah"