Kafara ya mfungaji aliyemjamii mkewe mchana wa Ramadhaan asiyeweza kulisha chakula

Swali: Je, kafara inadondoka kwa yule ambaye hakuweza kulisha chakula?

Jibu: Wanazuoni wamejengea hoja juu ya hili ya kwamba inadondoka na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Wape nacho familia yako.”

Hakumwamrisha kulipa. Kwa hiyo hilo likafahamisha juu ya kudondoka kwa kafara ya aliyemjamii mke wake ambaye hana uwezo. Hilo ni tofauti na kafara ya kumfananisha mke na mama au kafara ya kuua. Inabaki katika dhimma ya mtu mpaka mtu aitekeleze.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24163/هل-تسقط-الكفارة-عمن-لم-يستطع-الاطعام
  • Imechapishwa: 07/09/2024