Josho la janaba na wudhuu´ wa ambaye amefunga bendeji au amepaka rangi ya kucha

Swali: Je, inasihi kuoga janaba ikiwa vidole vina rangi ya kucha?

Jibu: Ikiwa kuna kitu juu yake kinapaswa kuondolewa  – ni mamoja rangi ya kicha au vinginevyo – vitu vilivyobandikwa ambavyo ni mchezo na visivyo na haja, hivyo vinaondolewa. Lakini bandeji, hupitisha juu yake maji. Lakini ikiwa ni rangi ya kucha au vitu vilivyobandikwa kwenye ngozi kama tope au unga wa kupika, basi vinaondolewa katika kuoga josho na katika kutawadha pia. Ama ikiwa ni kwa ajili ya sababu ya matibabu – kama vile jeraha au bandeji – hupitisha juu yake maji na yanatosha, au hupangusa juu yake ikiwa hawezi kutumia maji. Katika hali hiyo atapangusa na yanatosha kama wakati wa kutawadha. Lakini ikiwa ni vitu vilivyobandikwa visivyo na haja, kama rangi ya kicha, unga, tope au mfano wake, basi hivi vinaondolewa katika kuoga na vinaondolewa katika kutawadha pia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28044/حكم-الطلاء-والجبيرة-عند-الغسل-والوضوء
  • Imechapishwa: 07/04/2025