Josho la ijumaa linamlazimu ambaye ameamka kuchelewa?

Swali: Inajuzu kwa ambaye ameamka muda kidogo kabla ya swalah ya ijumaa aende kuswali bila kuoga?

Jibu: Tukikadiria kuwa mtu amesahau au amelala na asikumbuke wala asiamke isipokuwa muda kidogo kabla ya kuja kwa imamu kwa njia ya kwamba atachelewa iwapo ataoga, katika hali hii kunaanguka kwake kuoga. Kwa sababu kuoga josho la siku ya ijumaa ni kitaga na hivyo hatuwezi kupoteza msingi kwa sababu ya kitaga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1724
  • Imechapishwa: 10/05/2019