Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
“Enyi walioamini! Hakika si vyenginevyo pombe na kamari na kuabudu masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli ni uchafu kutokana na kazi ya shaytwaan, hivyo basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.”[1]
Hapa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anawazungumzisha waja Wake waumini kwa sababu wao ndio wako tayari kuitikia. Imani inakufanya kuweza kumuitikia Allaah (´Azza wa Jall). Ni wito wa utukufu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akaamrisha kuepuka na pombe na kamari. Maamrisho ya kuepuka jambo fulani ni makubwa zaidi kuliko pale inaposemwa tu mtu asifanye jambo fulani. Amri ya kukiepuka kitu maana yake ni kukiweka na kujitenga mbali nawe. Mkiepuka pombe basi litakupelekeeni kuweza kufanikiwa dhidi ya maadui wenu. Kama mnataka kufanikiwa nyinyi wenyewe, familia zenu na wengine wote, basi hakikishe mnajiweka mbali na pombe na kamari. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametamka kweli pale aliposema kuwa pombe inamuweka mbali mtu na Allaah na swalah. Kisha akasema:
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ
”Hakika si vyenginevyo shaytwaan anachotaka ni kutia baina yenu uadui na chuki, katika pombe na kamari na akuzuieni kumtaja Allaah na swalah, basi hivyo mtakoma?”[2]
Hapa wanazungumzishwa waumini. Ni kama kwamba waliitikia kusema: “Tumekoma!” Hata kam cheni yake ya wapokezi imekatika imesimuliwa kwamba ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alisema wakati kulipoteremshwa Aayah hiyo:
“Tumekoma, ee Mola!”
Kisha akasema:
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ
”Na mtiini Allaah na mtiini Mtume na tahadharini! Mkikengeuka, basi tambueni ya kwamba hakuna jengine juu ya Mtume Wetu isipokuwa kufikisha kuliko wazi.”[3]
Mtiini Allaah na Mtume Wake katika yale waliyokuamrisheni na msinywe pombe baada ya kutambua kuwa ni haramu:
فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ
” Mkikengeuka, basi tambueni ya kwamba hakuna jengine juu ya Mtume Wetu isipokuwa kufikisha kuliko wazi.”
Ni matishio makali. Mkipuuzilia mbali basi Allaah atawalipiza kisasi.
[1] 5:90
[2] 5:91
[3] 5:92
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 257-258
- Imechapishwa: 08/04/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 257-258
Imechapishwa: 08/04/2025
https://firqatunnajia.com/jiepushe-na-pombe-ili-uweze-kufanikiwa/