Je, Sunnah za Rawaatib zinakidhiwa?

Swali: Je, Sunnah za Rawaatib zinalipwa?

Jibu: Sunnah za Rawaatib zinalipwa pamoja na za faradhi. Hata hivyo hazilipwi zenyewe kama zenyewe isipokuwa Sunnah ya Fajr pekee ambayo inakidhiwa kwa iliyempita. Lakini ikiwa itampita swalah yaa faradhi pamoja na sunnah yake, kwa mfano Dhuhr, basi ataikidhi pamoja na sunnah yake, mfano mwingine ni Maghrib na ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24782/هل-يشرع-قضاء-السنن-الرواتب
  • Imechapishwa: 15/12/2024