Swali: Je, inahesabiwa kuwa ni shirki kwamba watu wengi hii leo wanaogopa zaidi kuvunja mipaka ya wanadamu, lakini hawakhofu kuvunja mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: Khofu imegawanyika katika aina tatu:
1 – Khofu ya siri. Hii ni shirki kubwa.
2 – Khofu ya kiumbe kwa mambo anayoyaweza, kama vile khofu ya mtawala dhalimu, majambazi au mwizi, hii haina tatizo. Mtu anachukua tahadhari. Allaah amesema kuhusu Muusa:
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ
“Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari.” (28:21)
Kwa maana ya kwamba alimwogopa Fir´awn na madhalimu wake.
Kwa hiyo mtu akimkhofia dhalimu na akaepuka shari yake au akakhofia majambazi akafanya ulinzi na kufunga milango, hakuna tatizo.
3 – Khofu ya kimaumbile, kama kuogopa baridi kali akavaa nguo za joto, kuogopa joto akatumia vitu vya kupoozea au kuogopa nyoka na nge akachukua tahadhar. Hii haina kosa lolote.
Swali: Wapo wanaoogopa zaidi kuvunja mipaka ya wanadamu lakini hawakhofu kuvunja mipaka ya Allaah?
Jibu: Iwapo khofu yao kwa wanadamu ni khofu ya kawaida yenye sababu, hiyo si shirki. Lakini ikiwa khofu hiyo inatokana na imani kwamba huyo wanadamu anajua mambo ya siri, ana uwezo wa kudhuru na kufaidisha kwa uwezo wake binafsi au anajua ghaibu, basi hiyo ni shirki. Ama khofu ya kimaumbile au ya kiakili kwa sababu ya dhuluma au tishio fulani, hiyo ni kama ile ya Muusa aliposema Allaah:
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ
“Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31154/هل-من-الشرك-الخوف-من-البشر
- Imechapishwa: 07/10/2025
Swali: Je, inahesabiwa kuwa ni shirki kwamba watu wengi hii leo wanaogopa zaidi kuvunja mipaka ya wanadamu, lakini hawakhofu kuvunja mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: Khofu imegawanyika katika aina tatu:
1 – Khofu ya siri. Hii ni shirki kubwa.
2 – Khofu ya kiumbe kwa mambo anayoyaweza, kama vile khofu ya mtawala dhalimu, majambazi au mwizi, hii haina tatizo. Mtu anachukua tahadhari. Allaah amesema kuhusu Muusa:
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ
“Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari.” (28:21)
Kwa maana ya kwamba alimwogopa Fir´awn na madhalimu wake.
Kwa hiyo mtu akimkhofia dhalimu na akaepuka shari yake au akakhofia majambazi akafanya ulinzi na kufunga milango, hakuna tatizo.
3 – Khofu ya kimaumbile, kama kuogopa baridi kali akavaa nguo za joto, kuogopa joto akatumia vitu vya kupoozea au kuogopa nyoka na nge akachukua tahadhar. Hii haina kosa lolote.
Swali: Wapo wanaoogopa zaidi kuvunja mipaka ya wanadamu lakini hawakhofu kuvunja mipaka ya Allaah?
Jibu: Iwapo khofu yao kwa wanadamu ni khofu ya kawaida yenye sababu, hiyo si shirki. Lakini ikiwa khofu hiyo inatokana na imani kwamba huyo wanadamu anajua mambo ya siri, ana uwezo wa kudhuru na kufaidisha kwa uwezo wake binafsi au anajua ghaibu, basi hiyo ni shirki. Ama khofu ya kimaumbile au ya kiakili kwa sababu ya dhuluma au tishio fulani, hiyo ni kama ile ya Muusa aliposema Allaah:
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ
“Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31154/هل-من-الشرك-الخوف-من-البشر
Imechapishwa: 07/10/2025
https://firqatunnajia.com/je-ni-katika-shirki-kuwaogopa-watu/