Je, Mitume watahojiwa ndani ya makaburi yao?

Swali: Je, Manabii, wakweli, mashahidi na watoto watahojiwa ndani ya makaburi yao?

Jibu: Allaah ndiye ajuaye zaidi. Kuhusu Manabii dhahiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba watahojiwa, kwa sababu Allaah amewalinda na kuwahifadhi. Ama wengine, basi kila mmoja atahojiwa isipokuwa watoto. Watoto hawakupewa jukumu la kufanya ´ibaadah. Kwa hiyo watoto hawana mahojiano, kwa sababu ´ibaadah haikuwa yenye kuwawajibikia. Lakini wengine kila mmoja atapewa mtihani ndani ya kaburi, isipokuwa Manabii (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), kwani inajulikana kuwa wao wamekingwa na kukosea.

Swali: Aliyekufa ndani ya kaburi atapewa mtihani?

Jibu: Zitazamwe Hadiyth zilizopokea kuhusu jambo hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31111/هل-يفتن-الانبياء-والشهداء-والاطفال-في-قبورهم
  • Imechapishwa: 02/10/2025