Je, Malaika humfunika ambaye anasikiliza Qur-aan au darsa?

Swali: Mtu anayesikiliza kanda ya Qur-aan ndani ya gari, muhadhara au  darsa – je, hufunikwa na Malaika?

Jibu: Hapana shaka yoyote kwamba hilo ni miongoni mwa kumtaja Allaah. Kanda ambayo ndani yake kuna kulingania kwa Allaah, mafunzo na miongozo ambayo anaisikiliza, au msomaji anayesoma na yeye akamsikiliza, hayo yote ni katika kumtaja Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31189/هل-تحف-الملاىكة-من-يستمع-الى-القران-والعلم
  • Imechapishwa: 11/10/2025