Je, kunaswaliwa ndani ya misikiti ambayo ndani yake ina makaburi?

Swali: Je, kunaswaliwa ndani ya misikiti ambayo ndani yake ina makaburi?

Jibu: Msikiti ulio na kaburi hakuswaliwi ndani yake, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amewalaani mayahudi na manaswara wameyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/233)
  • Imechapishwa: 01/03/2026