Je, kisomo cha Qur-aan ni bora zaidi kuliko Adhkaar katika kila wakati?

Swali: Nyuradi za wakati wake si zinatangulizwa mbele ya Qur-aan?

Jibu: Hakuna kikwazo. Bora zaidi ni kila kitu kukifanya ndani ya wakati wake. Lau utasoma Qur-aan ndani ya Rukuu´ umekatazwa kufanya hivo. Vivyo hivyo ndani ya Sujuud na baina ya Sujuud mbili. Qur-aan inasomwa mahala pake na Adhkaar mahala pake. Ni bora kila kitu kifanywe mahali pake. Hata hivyo hakuna ubishi ya kwamba ndio mazungumzo bora kabisa. Tukisema kwamba Qur-aan ndio mazungumzo bora kabisa haipelekei kwamba isomwe kwenye Sujuud, Rukuu´ na maeneo mengine ambayo sio ya kisomo. Kila ´ibaadah inafanywa mahala pake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24459/هل-تفضل-التلاوة-على-الاذكار-في-كل-وقت
  • Imechapishwa: 16/10/2024