Swali: Je, kiapo kizito (اليمين الغموس) kina kafara?

Jibu: Hakina kafara. Hata hivyo dhambi yake ni kubwa. Kafara inakuwa katika mambo mepesi ya masiku yajayo ambayo ameapa kwamba hatoyafanya kisha akayafanya, mambo ambayo ameapa kwamba atayaacha kisha akayafanya au kwamba hatoyafanya kisha akayafanya.

Kuhusu kiapo kizito ni khatari. Mtu akifanya hivo analazimika kutubia kwa Allaah na arudishe haki kwa mwenye nayo. Mfano wake ni mtu kuapa kwa Allaah kwamba mtu mwingine hamdai chochote ilihali anajua kuwa anadaiwa. Kwa mfano amemkopa 1000 SAR kisha baadaye mtu akaomba haki yake. Mdaiwa akaapa kwa Allaah kwamba mdai hamdai chochote. Mdai hana ushahidi kwa sababu alimdhania vizuri na hakuweka mashahidi dhidi yake. Hata hivyo mdaiwa akaapa kwa Allaah kwamba hakuna anachodaiwa. Hii ni aina miongoni mwa aina za kiapo kizito. Allaah akimjaalia arudishe haki kwa mwenye nayo na atubie kwa Allaah. Inatosha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24415/هل-لليمين-الغموس-كفارة
  • Imechapishwa: 08/10/2024