Je, inafaa kwa mtu anayeishi karibu na msikiti kumfata imamu msikitini?

Swali: Kuhusu mwanamke akiwa pembezoni na msikiti. Je, inafaa kwake kuswali pamoja na imamu ikiwa anasikia sauti yake?

Jibu: Hapana, aswali msikitini, aswali nyumbani kwake peke yake na asimfuate imamu ikiwa yuko mbali na msikiti. Ama ikiwa yupo msikitini au anamwona imamu au maamuma, hapana neno.

Mwanafunzi: Vipi ikiwa nyumba imekamatana na msikiti kama nyumba ya muadhini au nyumba ya imamu iliyoshikana na msikiti?

Ibn Baaz: Hata kama. Ikiwa hamwoni imamu wala maamuma, asimfuate, aswali peke yake.

Mwanafunzi: Je, bora zaidi mwanamke kuswali nyumbani kwake?

Ibn Baaz: Kuswali kwa wanawake majumbani mwao ndio bora zaidi.

Swali: Ikiwa watakuwa kundi la wanawake nyumbani mwao – je, waswali mkusanyiko au kila mmoja aswali peke yake?

Ibn Baaz: Jambo hili ni lenye wasaa. Wakitaka waswali wote pamoja na mmoja wao awaongoze, hili ni zuri; watajifunza na atawasomea Qur-aan na watasikiliza na kufaidika. Wakitaka kila mmoja aswali peke yake, jambo hili ni lenye wasaa.

Swali: Je, inajuzu ikiwa wanawake wanaswali ndani ya msikiti, lakini kuna kizuizi baina yao na wanaume?

Ibn Baaz: Ndio, hapana neno wakiwa ndani ya msikiti, muda wa kuwa wakisikia sauti, kama ilivyo msikiti wa Haram.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30900/هل-يجوز-للمراة-في-بيتها-ان-تقتدي-بامام-المسجد
  • Imechapishwa: 14/09/2025