Swali: Tofauti inayojulikana kuhusu mwenye kufa juu ya kufuru kunasemwa kwamba yuko Motoni?
Jibu: Aliyekufa juu ya kufuru, ni mamoja awe myahudi, mnaswara au mwingine, akifa juu ya dini yake basi yuko Motoni. Allaah amewatishia Moto. Kwa hiyo makafiri wako Motoni kwa yakini na waislamu wako Peponi kwa yakini.
Ama kuhusu mtu fulani kwa jina lake; fulani mwana wa fulani, hapa ndipo panapokuwa ni mahali pa kutazama. Je, inashuhudiwa kwake kwa jina au hapana? Isipokuwa yule aliyemshuhudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mayahudi wako Motoni. Manaswara wako Motoni. Makafiri wote wako Motoni. Ni kama ambavyo waumini wote wako Peponi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ
“Allaah amewaahidi waumini wanaume na waumini wanawake mabustani yapitayo chini yake mito.”[1]
Kwa hiyo kwa jumla wameahidiwa Pepo. Lakini inapokuja kwa fulani mwana wa fulani kwa sababu tu ni muumini, Allaah ndiye anayejua yaliyomo moyoni mwake. Isipokuwa yule aliyeshuhudiwa na ambaye amekingwa na kukosea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ameshuhudiwa Qur-aan, kama vile Abu Lahab:
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ
“Imeteketea mikono miwili ya Abu Lahab!”[2]
[1] 09:72
[2] 111:1
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31053/هل-يقال-لمن-مات-على-الكفر-انه-في-النار
- Imechapishwa: 26/09/2025
Swali: Tofauti inayojulikana kuhusu mwenye kufa juu ya kufuru kunasemwa kwamba yuko Motoni?
Jibu: Aliyekufa juu ya kufuru, ni mamoja awe myahudi, mnaswara au mwingine, akifa juu ya dini yake basi yuko Motoni. Allaah amewatishia Moto. Kwa hiyo makafiri wako Motoni kwa yakini na waislamu wako Peponi kwa yakini.
Ama kuhusu mtu fulani kwa jina lake; fulani mwana wa fulani, hapa ndipo panapokuwa ni mahali pa kutazama. Je, inashuhudiwa kwake kwa jina au hapana? Isipokuwa yule aliyemshuhudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mayahudi wako Motoni. Manaswara wako Motoni. Makafiri wote wako Motoni. Ni kama ambavyo waumini wote wako Peponi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ
“Allaah amewaahidi waumini wanaume na waumini wanawake mabustani yapitayo chini yake mito.”[1]
Kwa hiyo kwa jumla wameahidiwa Pepo. Lakini inapokuja kwa fulani mwana wa fulani kwa sababu tu ni muumini, Allaah ndiye anayejua yaliyomo moyoni mwake. Isipokuwa yule aliyeshuhudiwa na ambaye amekingwa na kukosea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ameshuhudiwa Qur-aan, kama vile Abu Lahab:
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ
“Imeteketea mikono miwili ya Abu Lahab!”[2]
[1] 09:72
[2] 111:1
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31053/هل-يقال-لمن-مات-على-الكفر-انه-في-النار
Imechapishwa: 26/09/2025
https://firqatunnajia.com/je-inafaa-kusema-kwamba-kafiri-fulani-yuko-motoni/