Swali: Je, inafaa kula nyama zinazotoka nchi za nje?
Jibu: Msingi juu ya nyama zinazotoka katika nchi za mayahudi na manaswara ni halali. Amesema (Ta´ala):
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ
“Leo mmehalalishiwa vizuri na chakula cha Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu.”[1]
Nchi za Ahl-ul-Kitaab ni zile za mayahudi na manaswara. Hata hivyo haitofaa kula ikiwa zimetoka katika nchi zisizokuwa za mayahudi na manaswara kama mfano wa nchi za wakomunisti.
Lakini kwa kuzingatia kwamba kumekuwa na mazungumzo mengi hii leo juu ya mitindo mbalimbali ya uchinjaji wa kisasa na kwamba wanachinja kwa kuwafanya wakazimia kwa umeme au kwa kuwanyonga, basi mtu anapaswa akae upande ulio salama zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Achana na linalokutia shaka na liendelee lisilokutia shaka.”
Hivi sasa – na himdi zote njema anastahiki Allaah – nchini mwetu wanachinja kwa njia ya Kiislamu. Njia ya Kiislamu ni kule kukata koo na umio kwa zana yenye makali. Aidha ni lazima mchinjaji awe muislamu, myahudi au mnaswara.
[1] 05:05
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
- Imechapishwa: 25/12/2020
Swali: Je, inafaa kula nyama zinazotoka nchi za nje?
Jibu: Msingi juu ya nyama zinazotoka katika nchi za mayahudi na manaswara ni halali. Amesema (Ta´ala):
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ
“Leo mmehalalishiwa vizuri na chakula cha Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu.”[1]
Nchi za Ahl-ul-Kitaab ni zile za mayahudi na manaswara. Hata hivyo haitofaa kula ikiwa zimetoka katika nchi zisizokuwa za mayahudi na manaswara kama mfano wa nchi za wakomunisti.
Lakini kwa kuzingatia kwamba kumekuwa na mazungumzo mengi hii leo juu ya mitindo mbalimbali ya uchinjaji wa kisasa na kwamba wanachinja kwa kuwafanya wakazimia kwa umeme au kwa kuwanyonga, basi mtu anapaswa akae upande ulio salama zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Achana na linalokutia shaka na liendelee lisilokutia shaka.”
Hivi sasa – na himdi zote njema anastahiki Allaah – nchini mwetu wanachinja kwa njia ya Kiislamu. Njia ya Kiislamu ni kule kukata koo na umio kwa zana yenye makali. Aidha ni lazima mchinjaji awe muislamu, myahudi au mnaswara.
[1] 05:05
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
Imechapishwa: 25/12/2020
https://firqatunnajia.com/je-inafaa-kula-nyama-zinazotoka-nchi-za-nje/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)