Je, inafaa kukata miti yenye kuudhi makaburini na kuweka miti au majani juu ya makaburi?

Swali: Je, inafaa kukata miti yenye kuudhi makaburini?

Jibu: Inatakiwa kukatwa. Kwa sababu inawaudhi wale watembeleaji. Vivyo hivyo ile miba inayopatikana huko ni inapaswa kuiondosha kwa ajili ya kuwapa amani watembeleaji kutokamana na shari yake. Haikusuniwa kwa yeyote kupanda juu ya makaburi mti au kuti aina lolote kwa sababu Allaah (Subhaanah) hakuweka Shari´ah hiyo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka makuti mawili juu ya makaburi mawili aliyokuwa anayajua na kwamba walikuwa wanaadhibiwa. Hakupanda juu ya makaburi mengine yaliyoko Madiynah na kwenye makaburi ya al-Baqiy´. Kadhalika Maswahabah hawakufanya hivo. Hivyo ikapata kutambulika kwamba kitendo hicho kilikuwa maalum kwa watu wawili wale waliokuwa wakiadhibiwa. Tunamuomba Allaah usalama.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/372) https://binbaz.org.sa/fatwas/922/%D9%82%D8%B7%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B4%D8%AC%D8%A7%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D8%B0%D9%8A%D8%A9-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%82%D8%A7%D8%A8%D8%B1
  • Imechapishwa: 07/12/2019