Swali: Ikiwa mwanafunzi amejishughulisha na kutafuta elimu na amehifadhi sehemu fulani ya Qur-aan na harejelei isipokuwa kile alichokihifadhi na anaacha yaliyobaki hadi Ramadhaan. Je hili linahesabika kuwa ni kuihama Qur-aan katika elimu wakati anasoma kila siku nusu juzu ya kile alichohifadhi?

Jibu: Tunamuomba Allaah kwamba hili lisihesabike kuwa ni kuihama. Lakini inampasa, ikiwa atapata nafasi, avute muda wake mpaka asome yaliyobaki kabla ya Ramadhaan. Kufanya hivo ndio bora zaidi. Vinginevyo hatuoni hili kuwa ni kuihama muda wa kuwa anajishughulisha na aliyokuwa nayo na anayashughulikia kwa kuyatafakari na kuyaweka katika hifdhi, hili ni jambo zuri. Lakini akipata nafasi ya kusoma yaliyobaki kabla ya Ramadhaan khitimisho moja au mbili au zaidi ya hivyo, basi hili ni bora kwake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1084/من-يقتصر-على-مراجعة-ما-يحفظ-من-القران-فقط
  • Imechapishwa: 23/01/2026