Je, hivi sasa hakuna haja ya kuchelewesha Dhuhr kwa sababu kuna viyoyozi na mafeni?

Swali: Mtu akisema kwamba sababu ya kuchelewesha swalah kwa ajili ya kupoa kwa joto ni kutokana na joto kali na sasa kuna viyoyozi vinavyondoa sababu hiyo?

Jibu: Haijalishi kitu. Sunnah haiwezi kubatilishwa, kwa sababu barabara hazina viyoyozi, barabara zina joto na hazina viyoyozi. Jengine ni kwamba si kila nchi ina viyoyozi.

Swali: Je, swalah inaweza kucheleweshwa zaidi kwa sababu joto linaweza kuendelea?

Jibu: Hadi joto lipungue. Baada ya nusu saa au zaidi kidogo, joto hupungua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27368/هل-يعمل-بالابراد-بالصلاة-مع-وجود-المكيفات
  • Imechapishwa: 23/03/2025