Je, anapata dhambi mwenye kuacha kuchinja Udhhiyah akiwa na uwezo?

Swali: Ni ipi hukumu ya Udhhiyah? Je, anapata dhambi mwenye kuacha kama ana uwezo?

Jibu: Hukumu ya Udhhiyah ni kwamba ni Sunnah kwa mwenye uwezo na sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo wawili wenye kunona. Maswahabah pia walikuwa wakichinja katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya kuaga kwake dunia. Vivyo hivyo waislamu baada yao. Haikupokelewa kwa mujibu wa dalili za Kishari´ah yanayofahamisha juu ya kwamba ni lazima. Maoni yanayosema kuwa ni lazima ni dhaifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/36)
  • Imechapishwa: 06/06/2024