Jamaa´at-ut-Tabliygh hawatilii umuhimu Tawhiyd kabisa

Swali: Kuhusiana na kisa ambacho kinasimuliwa na maimamu wa Da´wah ambapo wanasema namna baadhi ya Maswahabah walipata mwili wa Nabii Daaniyaal kisha wakalificha kaburi lake ili lisifanywe kuwa ni mahali pa kuswalia. Je, kisa hiki ni sahihi?

al-Albaaniy: Nini unachokusudia watu wa Da´wah?

Muulizaji: Mjukuu wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab.

 al-Albaaniy: Istilahi hiyo hii leo inatumiwa kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh.

Muulizaji: Hapana, sikuwakusudii wao.

al-Albaaniy: Najua hukuwakusudia wao, lakini mtu anaweza kufahamu hivo. Kwa ajili hiyo ndio maana nikashangazwa kutokana na nilivofahamu. Kwa sababu watu hawa hawatilii umuhimu mambo haya kabisa – mambo kuhusu Tawhiyd. Kwa hali yoyote, kisa ni sahihi na kina msingi uliyothibiti.

  • Mhusika: Imâm Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (304)
  • Imechapishwa: 14/05/2022