I´tikaaf haina muda wa chini

Swali: Ni muda gani wa chini kabisa wa I’tikaaf?

Jibu: Haina muda wa chini.

Swali: Mtu anaweza kukaa msikitini saa moja akakusudia I´tikaaf?

Jibu: Ndio, akinuia hilo[1].

[1] ´Abdur-Razzaaq (4/346) na Ibn Hazm (5/179) wamesimulia kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Abu Ya’la bin Umayyah ambaye amesema:

“Mimi wakati mwingine hukaa msikitini kwa muda wa saa moja na si kwa jengine isipokuwa kufanya I´tikaaf.”

´Abdur-Razzaaq amesimulia cheni yake mfano wa hayo kupitia kwa ´Atwaa´ na Ya´laa kutoka kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ni maoni ya Ibn Hazm na jopo la wanazuoni.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 129
  • Imechapishwa: 05/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´