ISIS ndio wamesababisha Islamophobia

Tuseme nini kuhusu watu hawa ambao wamelipua misikiti? Wamewaua wanawake, wamewaua watoto. Haya hayakutokea hata hapo zamani. Wanawaamrisha baadhi ya watu kujichimbia makaburi yao wenyewe. Wanawachoma moto na huku wengine wanatazama. Ni kama kwamba wamesoma madaftari ya namna ya kuadhibu.

Hawa bila shaka ndio wamesababisha yale yanayoitwa hii leo Uislamu wenye kukhofisha. Bi maana kuwa na khofu juu ya Uislamu. Haya ni mambo yaliyoenezwa na wamagharibi katika vyombo vyao vya khabari. Wameyasambaza kwenye magazeti yao wakiweka picha za ISIS ambapo wanachinja na kukata vichwa vya watu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Llc812dulFE&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 23/05/2019