Inatosha kuosha viungo vya wudhuu´ mara mojamoja

Swali: Je, inatosha kuingiza maji puani mara moja?

Jibu: Ndio.

Swali: Je, inatosha kuosha mkono mara moja pia?

Jibu: Ndio.

Swali: Je, vivyo hivyo kuhusu mguu?

Jibu: Ndio. Hata hivyo sahihi zaidi ni kwamba ni lazima kutawadha kwa kufululiza bila kukatisha na kupangilia. Kwa maana ya kwamba aanze kuosha uso, kisha mikono, kisha kupaka kichwa na hatimaye aoshe miguu. Anataka kupangilia viungo hivyo. Kwa ajili hiyo alimwamrisha (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) yule ambaye aliacha kufanya hivo aurudie wudhuu´ wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24719/هل-يصح-الاكتفاء-بمرة-واحدة-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 30/11/2024