Inatosha kueneza maji, si lazima kusugua mwili

Swali: Ikiwa mtu anaoga ili kujitwaharisha kutokana na najisi, kwa maana janaba, je, inamtosheleza kueneza maji katika mwili wake wote bila kuusugua?

Jibu: Maoni sahihi miongoni mwa maono ya wanazuoni ni kwamba kusugua mwili na viungo si faradhi katika wudhuu´ wala katika kuoga janaba. Kwa hiyo mwenye janaba anatosheka kumimina maji juu ya mwili wake mpaka yaenee mwili wote, na kumimina maji juu ya viungo vya wudhuu´ mpaka maji yavifikie vyote. Hata hivyo inapasa katika kuoga janaba kwanza kuosha najisi iliyoko kwenye tupu yake, kisha atawadhe kama anavyotawadha kwa ajili ya swalah, halafu amimine maji katika mwili wake wote mpaka yaenee mwili mzima. Wala haijuzu kumwita mwenye janaba kuwa ni najisi na wala kusema kwamba janaba ni najisi, kwa sababu imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema kuhusu mwenye janaba:

“Kwa hakika muislamu hanajisiki.”[1]

[1] al-Bukhaariy (01/333) na Muslim (01/282).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/323-324)
  • Imechapishwa: 26/11/2026