Swali: Ikiwa mtu ana janaba, kisha akakuta kisima, bwawa au bahari, akaingia humo na kuoga kwa nia ya kuondoa janaba – je, kuoga kwake kunamtosheleza?
Jibu: Ndiyo, kunamtosheleza ikiwa maji ni mengi kiasi kwamba yamefikia kiasi kisichopungua Qullatayn. Imepokelewa kwamba Ibn ´Umar amesema amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiulizwa kuhusu maji yanayopatikana katika maeneo ya nyika, ambayo wanyama wakali na wanyama wengine huenda kuyanywa, ambapo akasema:
“Yakiwa maji hayo yamefikia Qullatayn, basi hayabebi najisi.”[1]
Wameipokea maimamu watano wa Hadiyth. Imekuja katika riwaya ya Ibn Maajah na ya Ahmad:
“Hayapati najisi na chochote.”
[1] Ahmad (01/311), Abu Daawuud (01/17), an-Nasaa´iy (01/40), at-Tirmidhiy (01/97) na Ibn Maajah (01/172).
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/320-321)
- Imechapishwa: 26/11/2026
Swali: Ikiwa mtu ana janaba, kisha akakuta kisima, bwawa au bahari, akaingia humo na kuoga kwa nia ya kuondoa janaba – je, kuoga kwake kunamtosheleza?
Jibu: Ndiyo, kunamtosheleza ikiwa maji ni mengi kiasi kwamba yamefikia kiasi kisichopungua Qullatayn. Imepokelewa kwamba Ibn ´Umar amesema amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiulizwa kuhusu maji yanayopatikana katika maeneo ya nyika, ambayo wanyama wakali na wanyama wengine huenda kuyanywa, ambapo akasema:
“Yakiwa maji hayo yamefikia Qullatayn, basi hayabebi najisi.”[1]
Wameipokea maimamu watano wa Hadiyth. Imekuja katika riwaya ya Ibn Maajah na ya Ahmad:
“Hayapati najisi na chochote.”
[1] Ahmad (01/311), Abu Daawuud (01/17), an-Nasaa´iy (01/40), at-Tirmidhiy (01/97) na Ibn Maajah (01/172).
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/320-321)
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/maji-ambayo-mwenye-janaba-akiingia-kuoga-amesafika/