Inafaa kwa mwanamke kuweka sharti ya kutoolewa juu yake

Swali: Mke akimwekea sharti mume wake ikiwa ataoa mwingine juu yake basi amtaliki. Je, sharti kama hii inaenda kinyume na Shari´ah?

Jibu: Mwanamke yuko na khiyari endapo atamwekea sharti. Waislamu wako kwa sharti walizowekeana. Sharti inamfaa na kuoa kunamdhuru. Wanachuoni wamesema kwa uwazi kwamba inafaa kwake kuweka sharti na kwamba yuko na khiyari; akitaka, basi anaweza kumwacha, na akitaka anaweza kutengana naye kwa njia ya kwamba hahitajii kupewa talaka wala chochote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6171/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%B4%D8%AA%D8%B1%D8%A7%D8%B7-%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%A9-%D8%B9%D8%AF%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC-%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 16/10/2020