Inafaa kumjamii mke wangu baada ya ndoa kabla ya kumpa mahari?

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamume kumwingilia mke wake baada ya ndoa na kabla hajampa mahari?

Jibu: Ikiwa ndoa imetimia, basi hakuna ubaya hata kama mahari yamecheleweshwa. Ikiwa ndoa imetekelezwa baina yao, basi amehalalika kwake hata kama mahari yamecheleweshwa kwa miaka. Muhimu ni ndoa. Ikiwa ndoa imetekelezwa kwa masharti yake yanayozingatiwa na ikawa ni ndoa sahihi, basi inahalalika kwake hata kama mahari yamecheleweshwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1271/حكم-الدخول-على-المراة-بعد-العقد-وقبل-اعطاىها-الصداق
  • Imechapishwa: 14/02/2026