Swali: Vipi kuomba ulinzi kwa utukufu wa Allaah?
Jibu: Hii ni aina ya kujikinga na kufanya Tawassul:
أعوذ برضاك من سخطك، وبعفوك من عقوبتك، بعزة الله وقُدرته
”Naomba hifadhi kwa radhi Zako kutokana na ghadhabu Zako, kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, kwa utukufu wa Allaah na uwezo Wake.”
Lakini mtu asiseme:
“Ee utukufu wa Allaah! Tusaidie.”
Shaykh Taqiyyud-Diyn Ibn Taymiyyah amenukuu maafikiano ya wanazuoni kwamba sifa za Allaah haziombiwi. Kinachoombwa ni majina Yake tu.
Swali: Vipi kuhusu mtu kufanya Tawassul kwazo?
Jibu: Hapana vibaya kufanya Tawassul kwa sifa na kujikinga kwa sifa pia:
أعوذ بكلمات الله التامات، أعوذ برضا الله من سخطه، برضاك من سخطك
”Najikinga kwa maneno kamili ya Allaah, najikinga kwa radhi za Allaah kutokana na ghadhabu Zake, najikinga kwa radhi Zako kutokana na ghadhabu Zako.”
Lakini mtu asiseme:
”Ee radhi ya Allaah! Ee msamaha wa Allaah! Ee ujuzi wa Allaah! Ee usikivu wa Allaah!”
Badala yake aseme:
”Ee Allaah! Ee Msikivu! Ee Mjuzi! Ee Mpole! Ee Mwenye kurehemu, tusamehe na uturehemu!”
Allaah anaombwa kwa majina Yake:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
[1] 07:180
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31040/ما-حكم-التعوذ-بعزة-الله-والتوسل-بها
- Imechapishwa: 30/09/2025
Swali: Vipi kuomba ulinzi kwa utukufu wa Allaah?
Jibu: Hii ni aina ya kujikinga na kufanya Tawassul:
أعوذ برضاك من سخطك، وبعفوك من عقوبتك، بعزة الله وقُدرته
”Naomba hifadhi kwa radhi Zako kutokana na ghadhabu Zako, kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, kwa utukufu wa Allaah na uwezo Wake.”
Lakini mtu asiseme:
“Ee utukufu wa Allaah! Tusaidie.”
Shaykh Taqiyyud-Diyn Ibn Taymiyyah amenukuu maafikiano ya wanazuoni kwamba sifa za Allaah haziombiwi. Kinachoombwa ni majina Yake tu.
Swali: Vipi kuhusu mtu kufanya Tawassul kwazo?
Jibu: Hapana vibaya kufanya Tawassul kwa sifa na kujikinga kwa sifa pia:
أعوذ بكلمات الله التامات، أعوذ برضا الله من سخطه، برضاك من سخطك
”Najikinga kwa maneno kamili ya Allaah, najikinga kwa radhi za Allaah kutokana na ghadhabu Zake, najikinga kwa radhi Zako kutokana na ghadhabu Zako.”
Lakini mtu asiseme:
”Ee radhi ya Allaah! Ee msamaha wa Allaah! Ee ujuzi wa Allaah! Ee usikivu wa Allaah!”
Badala yake aseme:
”Ee Allaah! Ee Msikivu! Ee Mjuzi! Ee Mpole! Ee Mwenye kurehemu, tusamehe na uturehemu!”
Allaah anaombwa kwa majina Yake:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
[1] 07:180
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31040/ما-حكم-التعوذ-بعزة-الله-والتوسل-بها
Imechapishwa: 30/09/2025
https://firqatunnajia.com/inafaa-kujilinda-kwa-sifa-allaah-na-si-kuziomba-sifa/