Swali: Inafaa kwa mtu ambaye ana hali mbili zifuatazo kupokea zakaah? Hali ya kwanza anataka kuoa na hali ya pili ana kiwanja mpaka pale atapomiliki nyumba?
Jibu: Inajuzu kwake kupokea zakaah ikiwa hana uwezo wa kuoa, basi achukue zakaah, na ikiwa hana uwezo wa nyumba, inafaa kuchukua zakaah kwa ajili ya nyumba, ni mamoja kwa ajili ya kulipa kodi au thamani yake.
Swali: Je, ni ipi dalili ya hilo?
Jibu: Ufukara:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini…”[1]
Wale wasiokuwa na uwezo wa nyumba au jengo ni mafukara.
Swali: Mwanamke mmoja yuko ndani ya makazi na anasema kwamba mmiliki wa makazi anaweza wakati wowote kutufukuza na hatuna mahali pengine pa kwenda?
Jibu: Hapana, hapana ni mwenye kujitosheleza muda wa kuwa anayo makazi. Kifo kiko mikononi mwa Allaah.
Swali: Sio kwa sababu ya kuchelea kifo, ni kwa sababu ya kuchelea mmiliki kumfukuza.
Jibu: Akimfukuza atapokea zakaah.
Swali: Kwa hiyo sasa hivi asipokee?
Jibu: Akimfukuza atapokea zakaah.
[1] 09:60
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24658/حكم-اخذ-الزكاة-لمن-لا-يملك-كلفة-الزواج-والمسكن
- Imechapishwa: 19/11/2024
Swali: Inafaa kwa mtu ambaye ana hali mbili zifuatazo kupokea zakaah? Hali ya kwanza anataka kuoa na hali ya pili ana kiwanja mpaka pale atapomiliki nyumba?
Jibu: Inajuzu kwake kupokea zakaah ikiwa hana uwezo wa kuoa, basi achukue zakaah, na ikiwa hana uwezo wa nyumba, inafaa kuchukua zakaah kwa ajili ya nyumba, ni mamoja kwa ajili ya kulipa kodi au thamani yake.
Swali: Je, ni ipi dalili ya hilo?
Jibu: Ufukara:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini…”[1]
Wale wasiokuwa na uwezo wa nyumba au jengo ni mafukara.
Swali: Mwanamke mmoja yuko ndani ya makazi na anasema kwamba mmiliki wa makazi anaweza wakati wowote kutufukuza na hatuna mahali pengine pa kwenda?
Jibu: Hapana, hapana ni mwenye kujitosheleza muda wa kuwa anayo makazi. Kifo kiko mikononi mwa Allaah.
Swali: Sio kwa sababu ya kuchelea kifo, ni kwa sababu ya kuchelea mmiliki kumfukuza.
Jibu: Akimfukuza atapokea zakaah.
Swali: Kwa hiyo sasa hivi asipokee?
Jibu: Akimfukuza atapokea zakaah.
[1] 09:60
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24658/حكم-اخذ-الزكاة-لمن-لا-يملك-كلفة-الزواج-والمسكن
Imechapishwa: 19/11/2024
https://firqatunnajia.com/inafaa-kuchukua-zakaah-kwa-ajili-ya-kuoa-na-kulipa-kodi-ya-nyumba/