Imesihi kukusanya swalah wakati wa mvua kali

Swali: Ikiwa siku ina mvua na baridi kali, je, inaruhusiwa kukusanya swalah ya Dhuhr na ´Aswr pamoja (katika wakati wa ´Aswr)?

Jibu: Ikiwa kuna mvua inayowaletea watu uzito au kuna utelezi na matope katika njia, basi hakuna ubaya kukusanya kati ya swalah ya Dhuhr na ´Aswr, na kati ya Maghrib na ´Ishaa. Hii ni kwa sababu Sunnah na masimulizi sahihi kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) zimekuja zikithibitisha jambo hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/224)
  • Imechapishwa: 16/03/2026