Swali: Ikiwa kundi la wasafiri Dhuhr imewakuta katika mji njiani, kisha mmoja wa wasafiri akasimama kuwa imamu. Baada ya kuswali Rak´ah moja akachenguka wudhuu´ na kutoka na badala yake akasimama imamu mkazi. Je, wasafiri wamalize kwa Rak´ah ngapi, wakamilishe au wafupishe?
Jibu: Anayesimama baada yake atawaswalisha Rak´ah nne, nao watakamilisha naye. Kwa sababu maamuma anamfuata imamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru msafiri akiswali nyuma ya imaam mkazi aswali Rak´ah nne. Ibn ´Abbaas alipoulizwa kuhusu jambo hili alisema:
”Watu huswali nyuma ya imamu Rak´ah nne na wakiswali katika makazi yao wakiwa wasafiri huswali Rak´ah mbili.” Akasema: ”Hivi ndivyo Sunnah.”
Maswahabah wakati ´Uthmaan aliposwali kwa kukamilisha, nao walikamilisha pamoja naye ambapo wakaswali nne. Hivyo hawa ambao imamu wao amepatwa na hadathi na akaendelea mwingine akawakamilisha, basi wanaswali naye Rak´ah nne. Ikiwa ataanza nao swalah upya kuanzia mwanzo – kama walivyosema baadhi ya wanazuoni – basi ataanza nao na atawaswalisha Rak´ah nne, nao waswali naye Rak´ah nne. Akijengea juu ya ile ya kwanza na akaswali Rak´ah tatu, basi watakamilisha pamoja naye.
Swali: Lakini nia inatofautiana, kwa sababu wao walinuia kufupisha?
Jibu: Hata hivyo. Wanakamilisha pamoja naye. Mfano wake ni kama aliyeko katika merikebu au ndege, akaleta Takbiyr kwa nia ya swalah ya msafiri, halafu ndege ikatua katika mji wake, akawa ni mkazi. Katika hali hiyo ataswali kamili.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1099/كيفية-صلاة-المسافرين-اذا-استخلف-الامام-مقيما
- Imechapishwa: 15/02/2026
Swali: Ikiwa kundi la wasafiri Dhuhr imewakuta katika mji njiani, kisha mmoja wa wasafiri akasimama kuwa imamu. Baada ya kuswali Rak´ah moja akachenguka wudhuu´ na kutoka na badala yake akasimama imamu mkazi. Je, wasafiri wamalize kwa Rak´ah ngapi, wakamilishe au wafupishe?
Jibu: Anayesimama baada yake atawaswalisha Rak´ah nne, nao watakamilisha naye. Kwa sababu maamuma anamfuata imamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru msafiri akiswali nyuma ya imaam mkazi aswali Rak´ah nne. Ibn ´Abbaas alipoulizwa kuhusu jambo hili alisema:
”Watu huswali nyuma ya imamu Rak´ah nne na wakiswali katika makazi yao wakiwa wasafiri huswali Rak´ah mbili.” Akasema: ”Hivi ndivyo Sunnah.”
Maswahabah wakati ´Uthmaan aliposwali kwa kukamilisha, nao walikamilisha pamoja naye ambapo wakaswali nne. Hivyo hawa ambao imamu wao amepatwa na hadathi na akaendelea mwingine akawakamilisha, basi wanaswali naye Rak´ah nne. Ikiwa ataanza nao swalah upya kuanzia mwanzo – kama walivyosema baadhi ya wanazuoni – basi ataanza nao na atawaswalisha Rak´ah nne, nao waswali naye Rak´ah nne. Akijengea juu ya ile ya kwanza na akaswali Rak´ah tatu, basi watakamilisha pamoja naye.
Swali: Lakini nia inatofautiana, kwa sababu wao walinuia kufupisha?
Jibu: Hata hivyo. Wanakamilisha pamoja naye. Mfano wake ni kama aliyeko katika merikebu au ndege, akaleta Takbiyr kwa nia ya swalah ya msafiri, halafu ndege ikatua katika mji wake, akawa ni mkazi. Katika hali hiyo ataswali kamili.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1099/كيفية-صلاة-المسافرين-اذا-استخلف-الامام-مقيما
Imechapishwa: 15/02/2026
https://firqatunnajia.com/imamu-mkazi-amechukua-nafasi-ya-imamu-msafiri-na-kuwaswalisha-wasafiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket