Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Tunaonelea kuwa Sunnah imejengwa juu ya kushikamana na yale waliyokuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… “
Bi maana kushikamana na Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mfumo wa Mtume na makhaliyfah wake waongofu. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipozungumzia kuhusu mfarakano akataja kundi lililookoka na kusema:
“…. na Ummah wangu huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu; yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Kukasemwa: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kina nano hao?” Akasema: “Ni wale wenye kufuata yale ninayofuata mimi na Maswahabah wangu.”[1]
Tutapojua haya basi itamlazimu kila mwanafunzi kusoma kuhusu namna yalivyokuwa maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Bid´ah zilijitokeza baada yao ambapo baadhi ya za mwanzo ilikuwa Bid´ah za Khawaarij, Bid´ah za Raafidhwah, Bid´ah za Mu´tazilah, Bid´ah za Qadariyyah na kadhalika. Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiwakaripia kwa ukali. Katika “as-Swahiyh” ya Muslim imesihi ya kwamba Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alimwambia mtu aliyekuja kumweleza kuhusu Bid´ah za Qadariyyah:
“Ukikutana nao basi waambie kuwa mimi niko mbali na wao na kwamba wao wako mbali na mimi[2].
Baada ya hapo akawatajia Hadiyth kutoka kwa baba yake ambapo Jibriyl (´alayhis-Salaam) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Vilevile ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alikaripia Bid´ah za Khawaarij. Akamtuma binamu yake Ibn ´Abbaas ili kujadiliana nao. Matokeo yake elfutano katika wao wakarejea. Waliobaki wakaendelea kushikamana na madhehebu yao. Halafu akawapiga vita siku ya Nahrawaan[3].
Tunaona namna ambavyo Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walivyokemea na walivyokuwa wakichukia Bid´ah zilizokuwa katika wakati wao. Kinachothibitisha namna walivyokuwa wakichukia Bid´ah ni Hadiyth kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) inavyoeleza jinsi kiongozi wa Khawaarij alivyosulubiwa na kwamba ni mijibwa ya Motoni na kwamba ni viumbe waovu kabisa[4].
[1] Abuu Daawuud (4596) na at-Tirmidhiy (2641) kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (171).
[2] Muslim (8).
[3] ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (10/157).
[4] Ibn Maajah (176). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (3554).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 60-63
- Imechapishwa: 27/01/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)