Swali: Tunaomba umpe nasaha yule ambaye kafahamu kutoka katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Swalah ya ijumaa mpaka ijumaa nyingine ni yenye kufuta yaliyo baina yazo pale ambapo mtu ni mwenye kujiepusha na madhambi makubwa.”
Matokeo yake akawa anaacha swalah za mikusanyiko na huenda wakati mwingine akaacha swalah za faradhi au akazipuuza kwa matumaini kwamba swalah yake ya ijumaa ya pili inamfutia makosa hayo na khaswa khaswa baadhi ya ndugu zake wanaokuja. Tunataraji faida kutoka kwako.
Jibu: Faida ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Kuacha swalah ni dhambi kubwa. Bali baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa ni kufuru. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa mtu akiacha swalah moja tu mpaka ukatoka wakati wake pasi na udhuru, basi anakufuru. Hayo yamesemwa na wanachuoni wa kale na wa sasa kwamba kuacha swalah moja tu mpaka ukatoka wakati wake pasi na udhuru ni kufuru.
Kwa hiyo tunamwambia mtu huyu ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“… ni yenye kufuta yaliyo baina yazo pale ambapo mtu ni mwenye kujiepusha na madhambi makubwa.”
Ikiwa unataka kufahamu ufahamu huu, basi mimi nakuzidishia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“´Umrah mpaka ´Umrah nyingine ni yenye kufuta yaliyo baina yazo.”
Kwa hiyo usifunge na wala usiswali. Fanya ´Umrah peke yake. Kwani ´Umrah mpaka ´Umrah nyingine itakuwa ni kifutio. Hili pasi na shaka yoyote, ikiwa ni mjinga basi ni mjinga kweli na anatakiwa kujifunza. Na ikiwa ni mjuzi, basi ni mkaidi tu pasi na shaka.
Hakuna yeyote katika wanachuoni aliyefahamu kwamba kwa sababu ijumaa ni kafara/kifutio, basi inamwangushia mtu uwajibu wa swalah za mkusanyiko au uwajibu wa kuswali kabisa.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1064
- Imechapishwa: 17/03/2019

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1064
Imechapishwa: 17/03/2019
https://firqatunnajia.com/ima-ni-mjinga-au-mkaidi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)