Swali: Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Anayesema wakati wa asubuhi na wakati wa jioni:
سبحان الله وبحمده
”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake.”,
mara mia, hakuna atakayekuja siku ya Qiyaamah na bora zaidi kuliko alichokuja nacho isipokuwa mtu aliyeleta mfano wa alichosema au akaongeza juu yake.”
Je, idadi ya Tasbiyh hapa haikusudiwi kuwa imefungwa kwenye mia?
Jibu: Ndani yake kuna fadhilah kubwa. Kusema:

mara mia asubuhi na jioni ni miongoni mwa sababu za kusamehewa madhambi. Akiongeza na akasema mamia au maelfu, basi thawabu zake zitakuwa kubwa zaidi. Lakini sharti ni kusimama sawa katika dini. Fadhilah hizi zimefungwa na utekelezaji wa faradhi na kuacha yaliyoharamishwa. Kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa):
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا
“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Swalah tano, ijumaa moja hadi ijumaa nyingine na Ramadhaan moja hadi Ramadhaan nyingine ni kifutio cha madhambi yaliyopo baina yake iwapo atajiepusha na madhambi makubwa.”
Kwa hiyo fadhilah hizi zimefungwa na kuepuka madhambi makubwa na hivyo ndio Allaah hufuta madhambi madogo. Kuhusu mwenye kuendelea kwa makusudi kufanya maasi, basi ametishiwa kwa Moto hata kama ataleta na Tasbiyh na Dhikr, kwa sababu ya kuendelea kwake na maasi. Kama Alivyosema (Ta´ala):
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ
“Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, basi humdhukuru Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao – na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah? – na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua. Hao malipo yao ni msamaha kutoka kwa Mola wao na Pepo zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo – uzuri ulioje ujira wa watendaji wema!”[2]
Kwa hiyo ni wajibu kwa mja ajihadhari na yale aliyoyaharamisha Allaah, ajiepushe na kila kinachomghadhibisha Allaah, ashikamane na yale aliyoyamrisha Allaah, ajitahidi kuacha aliyoyaharamisha Allaah na alazimiane na tawbah kwa yale yaliyotangulia. Aidha imesuniwa kwake kufanya Tasbiyh, Tahliyl, Tahmiyd na takbiyr kwa wingi, kwani hayo ni miongoni mwa njia za kupata msamaha na miongoni mwa njia za kuongozwa.
[1] 04:31
[2] 03:135-136
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31024/هل-العدد-في-احاديث-الاذكار-توقيفي-لا-يزاد-عليه
- Imechapishwa: 29/09/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31024/هل-العدد-في-احاديث-الاذكار-توقيفي-لا-يزاد-عليه
Imechapishwa: 29/09/2025
https://firqatunnajia.com/idadi-ya-dhikr-kwenye-hadiyth-mbalimbali-ni-kwa-njia-ya-kukomeka/