Swali: Wasemaje kuhusu vijana wa sehemu ya mashariki mwa nchi ambao wanataka kuwalingania Raafidhwah katika haki wakatumbukia katika madhehebu yao. Waona mtu awakate au awalinganie?
Ibn ´Uthaymiyn: Wanataka kuwalingania Raafidhwah katika Sunnah?
Muulizaji: Ndio.
Ibn ´Uthaymiyn: Vipi wanataka kuwalingania katika Sunnah nao wanapita njia yao?
Muulizaji: Mwanzoni walikuwa hawataki kitu. Baada ya muda kuwa nao, wakabadilika na kuingia katika dini ya Raafidhwah.
Ibn ´Uthaymiyn: Wakawa nao Raafidhwah?
Muulizaji: Ndio. Hata baadhi yao wakawa wanasema wanaamini baraka za al-Husayn na wengine wanasema wanaweza kuwaozesha wasichana zao kwa Raafidhwah.
Ibn ´Uthaymiyn: Kwa vyovyote ni kuwa watu hawa wamepiga hatua nyuma kwa kuacha baya badala ya kuchukua kheri. Ni wajibu wao kutubu kwa Allaah na kurudi katika haki. Sisi tunashuhudia kuwa al-Husayn bin ´Aliy Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu) na kaka yake al-Hasan niviongozi wa vijana Peponi. Tunakubali fadhila zao na tunaona yaliyomfika ni mtihani kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Alisubiri na kuhesabu kulipwa kwa daraja ya wenye kusubiri. Lakini haijuzu kwa mtu kwa hali yoyote kuacha njia ya Salafiyyah na Sunniyyah na kuchukua madhehebu ya Bid´ah yanayokhalifu madhehebu ya Ahl-us-Sunnah. Watu hawa wakiendelea kwa waliomo baada ya kuwanasihi, ni wajibu kuwakata.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (167 A) Tarehe: 1418-06-15/1997-10-17
- Imechapishwa: 09/04/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)