Ibn ´Uthaymiyn kuhusu maiti kumjua anayekuja kumtembelea         

Kuhusu kufanya matembezi ya kuyatembelea makaburi maalum siku ya ijumaa au siku za idi ni kitu kisichokuwa na asli. Katika Sunnah hakuna kitu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinachofahamisha hayo.

Ama kuhusu maiti anamjua yule anayekuja kumtembelea, imekuja katika Hadiyth ambayo imepokelewa na Ahl Sunan na ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn ´Abdil-Barr na Ibn-ul-Qayyim akaafikiana naye katika kitabu chake “ar-Ruuh” ya kwamba mwenye kumsalimia maiti ilihali alikuwa anamjua duniani, basi hurudishiwa roho yake na maiti huyo akaitikia Salaam hiyo.

Ni wapi anasimama mwenye kuyatembelea makaburi? Anasimama sawa na kichwa cha maiti akimwelekea na huku aseme:

“as-Salaam ´alayk wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh. Ee Allaah! Msamehe, umrehemu na amuafu… “

Kisha amuombee kwa kile anachokitaka. Baada ya hapo aondoke. Hii ni mbali na ile du´aa ya jumla ambayo inasomwa wakati wa kuyatembelea makaburi kwa jumla inayosema:

 السَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحِقُـونَ، [وَيَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّا وَالْمُسْتَأْخِرِينَ] أَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ اللهم لا تحرمنا أجرهم، ولا تفتنا بعدهم، واغفر لنا وله

“as-Salaam ´alaykum! Enyi watu wa nyumba za watu waumini. Hakika sisi – Allaah akitaka – tutakutana na nyinyi. Allaah awarehemu waliotangulia katika sisi na nyinyi na wataokuja nyuma. Tunamuomba Allaah atuafu sisi na nyinyi. Ee Allaah! Usitunyime ujira wao, usitutie kwenye mitihani baada yao na utusamehe sisi na yeye.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (02)
  • Imechapishwa: 02/05/2020